This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.

Wednesday, February 06, 2008

Wakulima Same kuanza kulima zao la Jatrofa

Wakulima Same kuanza kulima zao la Jatrofa

2008-01-31 13:58:20
Na ITV Habari

Baadhi ya wakulima wa wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wamehamasika na kuanza kulima zao la Jatrofa baada ya mafuta ya zao hilo kuanza kutumika kuendeshea injini za magari.

Wakizungumza baada ya kuona gari linalotumia mafuta yanayotokana na zao hilo wakulima hao wamesema wamepata matumaini makubwa ya kuondokana na umaskini kupitia zao hilo jipya la biashara.

Naye mwakilishi wa shirika linalotengezeza mafuta hayo kutoka nchini Uholanzi Bw. Adjan Deoswijk amesema mafuta hayo ambayo pia hutumika kwenye mashine za kuzalisha umeme zikiwemo genereta yameonyesha uwezo mkubwa wa kuendesha injini za magari.

* SOURCE: ITV

No comments: