WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema changamoto kubwa inayoikabili wizara hiyo hivi sasa ni kupitia upya mkataba wa Kampuni ya Richmond iliyopewa zabuni ya kuzalisha umeme wa dharura.
Alisema ingawa kamati teule ya Bunge ya kuchunguza mkataba huo imetoa mapendekezo ambayo yanafanyiwa kazi chini ya waziri mkuu, wizara hiyo inapaswa kuupitia mkataba huo mapema kama sehemu ya utekelezaji wa mapendekezo hayo.
Katika mapendekezo, kamati hiyo iliyokuwa chini ya uenyekiti wa Mbunge wa Kyela, Dk. Harrison Mwakyembe, ilishauri pia kupitiwa kwa mkataba huo na mikataba mingine ya nishati nchini. Kamati hiyo imetoa muda wa miezi mitatu kwa serikali kutekeleza mapendekezo hayo.
Waziri Ngeleja alisema hayo jana katika hafla iliyoandaliwa na wafanyakazi wa wizara hiyo ya kuwakaribisha na kuwapongeza kwa kuteliwa, yeye pamoja na naibu wake, Adam Malima.
Alisema sambamba na changamoto hiyo, pia wizara hiyo inapaswa kuliimarisha Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), ili liweze kutoa huduma bora na za uhakika.
“Wizara yetu inakabiliwa na changamoto nyingi… tunapaswa kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme wa uhakika na yenye ubora. Kwa sasa hali ya maji katika Bwawa la Mtera ni nzuri na hata mvua zisiponyesha, yaliyopo yanaweza kutufikisha katika msimu mwingine wa mvua,”
Source: Tanzania Daima
This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.
Wednesday, February 20, 2008
Richmond sasa kuipasua kichwa wizara
Posted by
Godfrey
at
19:38
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment