This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.

Thursday, March 27, 2008

Ngeleja: Hakuna mgawo wa umeme

WAZIRI wa Nishati na Madini, William Ngeleja, amesema hakutakuwa na mgawo wa umeme mwaka huu.

Alitoa kauli hiyo alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana alipokuwa akizungumzia ugunduzi wa gesi asilia katika eneo la Uyuni, Mashariki mwa Kisiwa cha Songosongo wilayani Kilwa.

Alisema ipo mikakati ya makusudi ya kuzuia kuwapo kwa hali hiyo nchini licha ya maji yaliyopo kwenye vyanzo mbalimbali vya nishati hiyo muhimu kutosha kwa kipindi hiki.

“Hakuna mgawo wa umeme, kwa sasa maji yapo ya kutosha katika mabwawa yetu…kwa hali hii hatuutarajii mgawo kwa mwaka huu kabisa lakini pia tuombe Mungu hali isibadilike.

“Hali ya maji, mipango na mikakati yetu ipo vizuri, napenda kuwahakikishia kuwa hakuna mgawo mwaka huu,” alisisitiza Ngeleja na kuongeza kwamba, serikali inajitahidi kuzuia hali hiyo kama ilivyotokea mwaka 2006.

Siku saba zilizopita, Mkurugenzi wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), Idris Rashid, alikaririwa akitahadharisha kuwapo kwa mgawo wa umeme nchini.

Alisema kutokuwapo kwa mvua za kutosha ni moja ya sababu zitakazoleta mgawo wa umeme mwakani, licha ya shirika hilo kuhitaji sh trilioni 1.6 kwa ajili ya kujiimarisha kiuchumi.

Kuhusu gesi hiyo, alisema kampuni iliyoigundua ni Ndovu Resources Ltd kutoka Australia, yenye mkataba wa kutafuta mafuta ya petroli na gesi tangu Mei 19, mwaka 1999.

Alisema licha ya kugundua uwepo wa gesi hiyo, Kampuni ya Ndovu pia imechimba visima vitatu katika maeneo ya Uyuni, Kiliwani na Kiliwani North.

Alisema gesi hiyo iligundulika Machi 13 mwaka huu, kufanya visima vinavyotoa gesi nchini kufikia vinne katika maeneo mbalimbali nchini, yakiwamo yanayopakana na Bahari ya Hindi. Pamoja na Uyuni, maeneo mengine yaliyogunduliwa gesi ni Songosongo, Mnazi Bay na Mkuranga.

Katika hilo, alibainisha kwamba kutokana na ugunduzi wa visima hivyo vya gesi, serikali inaokoa kiasi kikubwa cha fedha zilizotakiwa kutumika kwa kuagiza mafuta ya dizeli nje ya nchi kwa ajili ya uendeshaji wa shughuli mbalimbali.

“Mfano katika mradi wa Songosongo kuanzia Juni 2004, gesi inayozalishwa inasaidia kutengeneza umeme kama nishati ya viwandani. Kiasi cha gesi kilichothibitishwa ni takriban futi za ujazo 540 bilioni.

Katika kipindi hiki taifa limeokoa dola za Marekani 992 milioni na vivyo hivyo katika mradi wa Mnazi Bay, ulioanza kuzalisha gesi ya ujazo wa futi 400 bilioni tangu Desemba mwaka 2006, umeokoa dola za Marekani 2.1 milioni,” alisema Ngeleja.

Mbali na hayo, alizungumzia mjadala wa wabunge kuhusu kukataliwa kwa muswada wa umeme na kufafanua kwamba, lengo si kubinafsisha Shirika la Umeme, badala yake ni kubadilisha sheria ya umeme ya mwaka 1931 ambayo imepitwa na wakati.

Aidha, aliitaka jamii ifahamu kwamba kupita au kutopita kwa muswada huo hakuhalalishi ubinafsishwaji wa TANESCO, na kuongeza kwamba wizara yake inaendelea kuufanyia marekebisho muswada huo.

Kuhusu dhana kwamba ipo faida inayopatikana kwa baadhi ya watendaji wa serikali ama wafanyabiashara, Waziri Ngeleja alikanusha na kusema uharakishwaji wa muswada huo unatokana na masilahi yake kwa jamii na taifa kwa jumla.

“Wapo baadhi ya watu wanadhani kwamba, kuna jambo nyuma ya pazia, lakini hakuna kitu, tunaipenda nchi yetu na tunafanya hivi kwa manufaa ya taifa kutokana na muswada uliokuwapo wa mwaka 1931 kupitwa na wakati. Mara zote unafanyiwa marekebisho lakini hayatoshi,” alisema Ngeleja.

Alisema, hivi sasa TANESCO linajiendesha kibiashara zaidi, hali iliyosababisha serikali kukatisha ruzuku kwa shirika hilo. Hivyo hata sheria ikipitishwa halitabinafsishwa.

Alisema: “Wizara inazingatia mapendekezo ya wabunge na itayafanyia kazi, lakini napenda wananchi waelewe kuwa Shirika la Umeme halitabinafsishwa na wala hakuna chochote nyuma ya pazia kuhusu muswada huu.”

Source: Tanzania Daima, 27/03/2008

Serikali yautetea Muswada wa sheria ya Umeme

WIZARA ya Nishati na Madini imemsafisha aliyekuwa waziri wake Nazir Karamagi na kusema, hakuna msukumo wowote wa kifisadi katika kutengeneza muswada wa Sheria Mpya ya Umeme na Mafuta ya Petroli unaotarajiwa kuwasilishwa Bungeni mwezi ujao.

Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja alisema jana jijini Dar es Salaam kuwa fikra zilizojengeka kwamba kuna ujanja katika kutengeneza muswada huo hazina mantiki wala ukweli wowote.

"Wazo kwamba kuna kitu 'nyuma ya pazia' katika kutengeneza muswada huo ni potofu. Napenda kuueleza umma na ndugu zangu (waandishi) mnisaidie kwamba sio kweli, wizara inafanya hivyo kwa maslahi ya Taifa, kusiwe na wazo kwamba msukumo huo wa muswada wa Sheria mpya ya Umeme una maslahi kwa mtu," alisema Ngeleja.

Kauli ya Ngeleja imekuja juma moja tangu wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania waukatae tena muswada huo wenye lengo la kufungua milango kwa wawekezaji wa nje kuwekeza katika sekta ya umeme wakidai kuwa bado una harufu ya aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi.

Ngeleja aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa kukataliwa kwa muswada huo kwa sababu yoyote ile, hakutaondoa umuhimu wa kuifanyia marekebisho sheria ya umeme ya mwaka 1931 ambayo kulingana na mabadiliko ya kijamii, imepitwa na wakati.

"Sheria hii ya Umeme ilitungwa mwaka 1931 na ina upungufu mwingi, ni lazima ifanyiwe marekebisho ili iende na wakati,"alisisitiza Ngeleja na kuendelea:

"Hoja kwamba sekta binafsi kwenye umeme itakwamisha mpango wa serikali kupeleka nishati hiyo vijijini siyo kweli kwani hata Tanesco haiwajibiki kupeleka umeme vijijini,"

Alisema hoja hiyo imepitwa na wakati kwani hata Tanesco haiwajibiki kupeleka umeme vijijini bali Serikali kupitia Wakala wa Umeme vijijini (REA) katika mkataba ulioingiwa mwaka 2005.

"Tutunge sheria hii au tusitunge, Tanesco siyo suluhu la tatizo la umeme vijijini, kazi hiyo ni ya serikali kupitia Wakala wa Kusambaza Umeme (REA) tangu mwaka 2005," alisema.

Alisema katika muswada huo wa sheria hiyo mpya, serikali imejitahidi kukwepa kubinafsisha huduma ya umeme kwenye maeneo yanayoweza kuliathiri taifa kama ubinafsishaji wa miundombinu yake.

Alieleza kuwa katika sheria hiyo mpya serikali iliruhusu uwekezaji katika uzalishaji na usambazaji wa umeme maeneo ambayo tayari yamekuwa yakiendeshwa na kampuni za nje.

"Sisi tunaruhusu soko huria katika uzalishaji na usambazaji na siyo usafirishaji na hili sio jambo geni kwani hata sasa maeneo haya tayari yako huru kwa wawekezaji,"alisema.

Hata hivyo alibainisha kuwa kauli za wabunge hao kuhusu muswada huo hazikutolewa ili kuukubali wala kuukwamisha bali ni mapendekezo yatakayotumika kuuboresha zaidi kabla haujaingia bungeni.

"Kukataliwa kwa Muswada huo ni changamoto kwa serikali katika kuuboresha zaidi kwani hayo ni mapendekezo tu na sio msimamo wa mwisho wa wabunge," alisema.

Wabunge hao walionyesha kukerwa na muswada huo katika mjadala uliofanyika Machi 18 mwaka huu jijini Dar es Salaam kuhusiana na mapendekezo ya serikali kutunga sheria mpya ya umeme itakayoruhusu uwekezaji katika sekta hiyo.

Wabunge hao walisema hawajaona tofauti yoyote katika muswada huo na uliowasilishwa mara ya kwanza ambao ulipitiwa na kutolewa mapendekezo ya mabadiliko katika baadhi ya vipengele. chini ya aliyekuwa na waziri wa wizara hiyo, Nazir Karamagi

Walisema muswada huo pia hauonyeshi mpango wowote wa kuweka umeme maeneo ya vijijini ambako ndio kuna wananchi wengi.

Mbunge wa Karatu Dk Willibrod Slaa alitoa angalizo kuwa kwa sasa hakuna kampuni yoyote ya uwekezaji inayoweza kupeleka umeme vijijini na kuitaka serikali kuhakikisha inatekeleza jukumu hilo yenyewe na kuongeza kuwa kuukubali mswada huo ni sawa na kuiweka nchi mikononi mwa wawekezaji.

Source: Mwananchi, 27/03/2008

Thursday, March 06, 2008

Rural-Connectivity-Tz-2007-Suhail-Sheriff.pdf (application/pdf Object)

Reliable power backup system is required in order to operate ICT systems and to ensure that they continue operating during critical periods. The consequences of power cuts can be more severe for sensitive sensitives such as Health Management Information System HMIS in large hospitals where patient healthcare depends on a well-functioning ICT system.

Connectivity and use of ICT facilities is rendered useless without adequate power supply. More about the importance and how to develop reliable power supply, please read a complete report at:
Rural-Connectivity-Tz-2007-Suhail-Sheriff.pdf (application/pdf Object)

Saturday, March 01, 2008

Richmond yaibua makubwa TANESCO

WAFANYAKAZI wa Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (TANESCO), wametishia kuwaburuza mahakamani watu walioingia mkataba wa kuzalisha umeme wa dharura kati ya shirika hilo na Kampuni ya Richmond.

Aidha, wafanyakazi hao wametaka kusimamishwa malipo kwa Kampuni ya Dowans iliyorithi mkataba huo.

Wafanyakazi hao walitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa kujadili masuala mbalimbali ya shirika hilo na kueleza kushangazwa na kitendo cha kuendelea kuilipa kampuni ambayo msingi wake unatokana na mkataba uliohusisha kampuni hewa.

Mwenyekiti wa kamati ya majadiliano ya wafanyakazi hao, Abdul Mkama, alisema hakuna sababu kwa Tanesco kuendelea kuilipa shilingi milioni 152 kwa siku, kampuni ambayo imedhihirika kuwa ilishinda zabuni kifisadi.

Sambamba na hayo, alisema ni vema watu waliojiuzulu wakarudisha fedha hizo kama inavyofanyika kwa watu waliochukua fedha katika akaunti ya malipo ya nje (EPA), na baada ya kufanya hivyo, wakafikishwa kwenye vyombo vya sheria.

“Sisi wafanyakazi wa Tanesco, tunataka malipo yanayofanyika kwa Richmond yasimamishwe kuanzia leo (jana), na tunafanya taratibu, ili wahusika watulipe fidia, wasipofanya hivyo tutawaburuza kwenye vyombo vya sheria,” alisema Mkama.

Naye, Balton Mwaifugile, alisema viongozi waliojiuzulu ni sehemu ndogo ya mafisadi, hivyo ni vema waliobakia nao wakaanikwa hadharani, ili kukomesha tabia ya kufuja mali za umma kwa maslahi binafsi.

Alisema wanachohitaji wao ni kulipwa fidia kwa hasara iliyopatikana, kwani fedha hizo ni nyingi na zingewasaidia kuboresha maisha yao na mitambo ya shirika hilo.

“Tunawalipa hawa jamaa wa Richmond milioni 152 kwa siku, Songas milioni 200 kwa siku na IPTL sh bilioni tatu kwa mwezi. Fedha hizi ni nyingi, na kuanzia leo tunataka tuanze kuwashughulikia kwa kutowapa fedha,” alisema Mwaifugile.

Alisema maisha ya wafanyakazi yamekuwa magumu na kupata majanga mbalimbali yaliyowasababishia ulemavu, huku wakilipwa fidia kidogo kwa madai shirika halina uwezo wa kuwalipa kutokana na fedha nyingi kuchukuliwa na mafisadi.

“Kabla ya ‘kuwanyonga’ mafisadi wetu, kwanza watulipe fidia kutokana na matatizo waliyotusababishia, ili na sisi tuishi kwa raha na kuendesha magari kama wanavyofanya wao na familia zao,” alisema Mwaifugile.

Kwa upande wake, John Mwandika, alisema hivi sasa kuna bomu kubwa linakuja nchini, kwani mradi wa kuzalisha makaa ya mawe ya Kiwira nao unatarajia kuanza kulipwa sh milioni 300 kwa siku utakapoanza uzalishaji.

Alisema mradi huo wa Kiwira utakuwa unatumia sh bilioni tisa kwa mwezi, gharama ambazo zinadaiwa zitabebwa na Tanesco, ambayo inaonekana mnyonge na sehemu ya kuchuma.

“Tanesco imefanywa mti wa mzambarau, kila mtu anakuja na kapu lake na kutingisha matunda, na kapu linapojaa huondoka na matunda,” alisema Mwandika.

Aidha, Thomas Njama, alisema wabunge wa Tanzania ni waoga, kwani suala la ubadhirifu katika Tanesco lilianza kwa menejimenti ya Net Group Solution ambayo kwa kiasi kikubwa ilivuruga muundo mzima wa shirika hilo.

Alisema uongozi huo kwa kushirikiana na serikali ya awamu ya tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, wamefanikiwa kuuza majengo mbalimbali ya Tanesco, ikiwepo kutoa Chuo cha Morogoro na kuuza kiwanda cha kukaanga nguzo kilichopo Mbeya.

Aidha, alisema ni vema kuanzia sasa Katiba ya Tanzania ikabadilishwa, ili kuweza kuwakamata marais ambao watakuwa wamefuja mali za umma kwa maslahi binafsi.

Alisema Mkapa alikuwa kinara wa kushinikiza mabadiliko katika shirika hilo kwa maslahi ya watu wachache, bila kuangalia athari kwa taifa.

“Hii katiba inayotoa kinga ya kutowashtaki marais pindi wanapondoka madarakani imepitwa na wakati, inafaa tuibadilishe, ili tuweze kumkaanga Mkapa,” alisema Njama.

Source: Tanzania Daima, 01/03/2008

Richmond yawatia nyongo Tanesco

*Wataka viongozi waliosaini mkataba washitakiwe haraka
*Wadai wanachangia kuiua kwa mikataba mibovu, gharama

WAFANYAKAZI wa Shirika la Umeme (Tanesco) wamecharuka na kutaka viongozi na watendaji wengine serikalini walioliingiza shirika hilo katika hasara kwa kusaini mkataba na kampuni ya kuzalisha umeme wa dharura ya Richmond, washitakiwe haraka.

Katika mkutano wao uliofanyika mapema leo makao makuu, wafanyakazi hao walisema baadhi ya viongozi ndani ya serikali wamekuwa mstari wa mbele kuhakikisha Tanesco inakufa, ndiyo maana wanaliingiza kwenye mikataba waliyoiita ya kinyonyaji.

“Yaani Tanesco imegeuzwa mwarobaini, kila mtu analeta mkataba wake ili anyonye na kuondoka,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Majadiliano ya Tanesco, Abdul Mukama.

Alisema mkataba wa Richmond ambao ulipigiwa kelele na wafanyakazi wa shirika hilo, unadhihirisha namna viongozi wa siasa walivyodhamiria kuhakikisha shirika hilo linakufa kutokana na fedha zinazolipwa na shirika hilo kwenda kwenye kampuni binafsi.

Mukama alisema wafanyakazi kwa muda mrefu wamekuwa wanajituma kuhakikisha shirika hilo linainuka, lakini tangu serikali iingie mkataba na kampuni ya IPTL, Songas, Aggreko na sasa Richmond, zimekuwa zinalipwa fedha nyingi na shirika hilo.

“Mimi sioni kama hawa walistahili kujiuzulu, hawa wanatakiwa kukamatwa na kushitakiwa haraka,” alisema Mukama wakati akifungua mkutano huo ambao ulikuwa unajadili suala hilo la mkataba wa Richmond.

Mukama alisema mtu wa kwanza ambaye alitaka kuiua Tanesco ni Rais mstaafu Benjamin Mkapa, ambaye aliingiza menejimenti ya Afrika Kusini kwa nguvu ambayo pia haikuleta ufanisi wowote zaidi ya kuuza mali za shirika hilo na kuliacha likiwa hoi kifedha.

Alisema Rais Mkapa aliipeleka Tanesco kwa dalali ambaye ni Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma (PSRC) kwa miaka 10. Alisema katika kipindi hicho shirika hilo halikuruhusiwa kuingia katika mkataba wa aina yoyote ile mkubwa, hali iliyosababisha miundombinu yake kuchakaa.

Baadhi ya wafanyakazi wengine ambao walipata fursa ya kuchangia kwenye mkutano huo, walisema viongozi wa siasa wakiwamo wale ambao wameingia mkataba wa Richmond, wameshiriki kuidhoofisha Tanesco.

“Rais Kikwete ameelemewa na ufisadi wa watangulizi wake. Haya yanayofanyika ndani ya Tanesco yameanza siku nyingi, anashindwa afanye nini kama anataka kusafisha uozo, ni vyema pia amshitaki Rais mstaafu,” alisema Thomas Njumayo.

Walisema kitendo cha kampuni ya Richmond na sasa Dowans kulipwa Sh bilioni 4.7 kwa mwezi na Tanesco inaonyesha namna ambavyo viongozi wa siasa wasivyokuwa na uchungu na shirika hilo.

Mfanyakazi mwingine alisema ni vyema serikali iilipe fidia Tanesco kwa vile katika miaka minane shirika hilo limeathirika kwa kiasi kikubwa, ikiwamo kupoteza chuo chake cha Morogoro kilichokuwa kinatoa wataalamu wa hali ya juu.

Alisema pia Tanesco inatakiwa kulipwa faida, kwa vile menejimenti ya Netgroup iliuza baadhi ya majengo katika hali ya kutatanisha, huku wakiliacha shirika likiwa katika hali mbaya ya fedha.

Mfanyakazi mwingine aliyejitaja kwa jina la Mwakugile alitaka wafanyakazi hao waazimie kama fedha hizo zinalipwa kutoka hapo Tanesco wazizuie, ziweze kuongeza ufanisi wa shirika hilo.

Suala la Richmond lilitokana na ripoti ya Kamati teule ya Bunge iliyokuwa inaongozwa na Dk Harisson Mwakyembe ambayo ilibaini namna ambavyo baadhi ya viongozi, akiwamo aliyekuwa Waziri Mkuu Edward Lowassa, aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi na Dk. Ibrahim Msabaha kujiuzulu.

Wafanyakazi wa Tanesco walisema jana kwamba viongozi hao wameshiriki katika kulidhoofisha shirika hilo, hivyo wanastahili kushitakiwa na siyo kujiuzulu tu.

Source: Habari Leo, 29/02/2008

Blackout caused no deaths– Muhimbili

THE management of Muhimbili National Hospital has refuted reports that five infants died at midnight on February 27 this year following power cut. The statement issued today by the hospital’s head of Relations Unit Aminiel Aligaesha said the reports by a daily tabloid were unfounded and untrue.

The daily tabloid ran the story today that five infants including two infants who were born prematurely died on the said day after a power cut and a delay to start standby generators.

“There’re no machines which use electricity in a ward which accommodated the premature infants. There’s no child who died due to the power cut as alleged by the newspaper,” read part of the statement.

However, Aligaesha admitted that there was a power cut on that night and Tanesco restored it on February 28 around 1.30pm. “The hospital has six standby generators and they were all switched on during that night until today (February 28) at 9.00 in the morning.” The statement said.