Riroti ya Kamati ya Bunge ya kuchunguza mkataba wa Richmond inayosubiriwa na Watanzania wengi kujua kilichomo inatarajiwa kuanza kugawiwa kwa wabunge leo tayari kwa kujadiliwa muda wowote kuanzia sasa.
Habari ambazo hazikuthibitishwa jana, zilisema kuwa huenda ripoti hiyo ikaanza kujadiliwa na wabunge wa CCM leo katika vikao vyao vya siri.
Habari za uhakika zilizopatikana bungeni jana jioni zilisema kuwa wabunge wote wanatarajiwa kugawiwa ripoti hiyo ili waisome tayari kwa kuijadili.
Hatua hiyo imekuja baada ya Spika wa Bunge, Bw. Samwel Sitta, kusitisha safari ya kikazi ya kwenda Marekani.
Taarifa za kusitisha safari hiyo zilitangazwa Bungeni juzi na Naibu Spika, Bi. Anne Makinda ambapo, hata hivyo, hakutoa sababu zilizomfanya Spika Sitta kufuta ziara yake aliyopanga kuondoka juzi.
Wiki iliyopita Bw. Sitta aliwaaga wabunge kuwa hatohudhuria vikao vya Bunge kwa wiki nzima kwa vile atakuwa nchini Marekani, kisha akazuia kuwasilishwa na kusikilizwa kwa ripoti ya Richmond hadi hapo atakaporejea.
Pia alizuia kujadiliwa kwa ripoti ya upotevu wa mamilioni ya pesa Benki Kuu ya Tanzania (BoT) bila yeye kuwepo.
Bw. Sitta alitoa kauli hiyo kwa maelezo kwamba masuala hayo ni nyeti na kwamba yanapaswa kujadiliwa akiwepo.
Katika hatua ambayo haikutarajiwa, majuzi wabunge walisusia semina ya miswada ya sheria za nishati (umeme na mafuta) iliyoandaliwa na Waziri wa Nishati na Madini, Bw. Nazir Karamagi.
Wabunge hao kwanza walitaka wafahamu kilichomo kwenye ripoti ya Richomond ndipo wajadili umuhimu wa mabadiliko yatakayoletwa na sheria hizo mpya.
Source: The Guardian, 6/2/2008
This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.
Wednesday, February 06, 2008
Moshi wa Richmond wafukuta
Posted by
Godfrey
at
14:23
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment