This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.

Thursday, October 25, 2007

Karamagi asisitiza umuhimu wa tekinoljia isiyoathiri mazingira

Karamagi asisitiza umuhimu wa tekinoljia isiyoathiri mazingira
Na Milton Nyirenda, Arusha

MATUMIZI ya nishati mbadala yanayozingatia teknolojia isiyoathiri mazingira ni miongoni mwa njia pekee zinazoweza kuongeza kasi ya maendeleo ya kiuchumi na kukwamua idadi kubwa ya wananchi wanaoishi vijijini barani Afrika.

Kauli hiyo, ilibainishwa na waziri wa Nishati na Madini,� Nazir Karamagi kwenye� mkutano wa kimataifa wa maendeleo na nishati barani Afrika uliofanyika katika hoteli ya kitalii ya Ngurdoto nje kidogo ya jiji la�Arusha.


Karamagi alisema kuwa katika nchi za kusini mwa Jangwa la Sahara ni asilimia tano tu ya wananchi wanaoishi vijijini wanaopata umeme wa gridi na kwamba Tanzania ikiwa miongoni mwa nchi hizo wananchi chini ya asilimia mbili wanatumia nishati ya umeme katika maeneo ya vijijini.


Aliwataka washiriki wa mkutano huo wa siku tatu kufanya tathimini ya kina katika kubaini mapungufu ya miradi ya nishati vijijini inayoendeshwa na nchi sita barani Afrika kwa ushirikiano na serikali za Denmark na Uholanzi ili kuboresha maisha ya wananchi wa vijijini.

Karamagi alisema ili kupunguza umaskini na kuleta mapinduzi ya kiuchumi katika maeneo ya vijijini ni muhimu kujenga miundo mbinu ya uzalishaji wa nishati mbadala itakayochochea viwanda vidogo vidogo na pia kuwapa wananchi fursa ya kuboresha mazao yao.

Kuhusu kupungua kwa kasi ya kujenga miundo mbinu ya usambazaji wa umeme vijijini kwa miaka kumi iliyopita, waziri alisema serikali ilikuwa ikiandaa utaratibu wa kubinafsisha shirika la umeme (Tanesco),

Alisema mpango huo umesitishwa na badala yake serikali inahakikisha kuwa kasi ya kusambaza huduma hiyo kwenye maeneo hayo inaendelezwa ingawa kinachotakiwa ni wananchi kutumia nishati hiyo kibiashara kwa maendeleo yao.

Kwa upande wake meneja wa taasisi ya nishati mbadala ittwayo TATEDO Oscar Lema alisema kuwa taasisi hiyo ilianza kuonyesha matukio katika baadhi ya mikoa ambapo katika wilaya za Monduli na Arumeru imekwisha funguliwa miradi ya uzalishaji wa nishati inayotengenezwa kutokana na zao la Jatrofa.

Ametaja vituo vinavyozalisha umeme huo kuwa ni Longido wilayani Monduli na Leguruki katika wilaya ya Arumeru.

Source: Mwananchi Mwananchi Communication Limited (MCL)

No comments: