Source: Tanzania Daima, 14/11/2007
SHIRIKA la Ugavi Tanzania (TANESCO) kwa ushirikiano na Serikali, linatayarisha mikataba ya msingi ya kununua na kuuziana umeme kwa kupanga bei za umeme katika miradi midogo itakayouza nishati hiyo kwenye gridi ya taifa.
Hayo yalielezwa na Naibu Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, alipokuwa akijibu swali la msingi la Mbunge wa Hai, Fuya Kimbita (CCM), aliyetaka kujua mikakati ya kuvifufua vituo vidogo vilivyozalisha umeme siku za nyuma katika baadhi ya maeneo nchini.
Alisema, lengo la kuanzisha utaratibu huo ni kuboresha na kurahisishia kampuni binafsi kushiriki katika miradi midogo ya umeme kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa huduma ya hiyo na kuongeza kasi ya kuwapelekea wananchi wengi mjini na vijijini huduma hiyo.
Awali, TANESCO ilipokea maombi kutoka kwa baadhi ya kampuni binafsi zenye nia ya kufufua vituo vidogo vya kuzalisha umeme wa maji vya Kikuletwa, Tosamaganga na Mbalizi ambapo shirika hilo lilitangaza zabuni hiyo.
Ngeleja, alisema tathmini ya zabuni hiyo ilionyesha kuwa bei za umeme zilizopendekezwa na wazabuni zilikuwa juu hivyo zingesababishia TANESCO kununua umeme huo kwa hasara.
"Kutokana na mazingira ya sasa kuwa tofauti na ya wakati ule ambapo ilionekana ni vigumu kwa shirika hilo kuingia mikataba na wazabuni waliojitokeza kwa sasa shirika hilo na Serikali wanaanzisha utaratibu huu mpya," alisema Ngeleja.
Alisema, baada ya kukamilika kwa utaratibu huo Tanesco watatangaza zabuni ya kupata kampuni bora ambazo zitaendeleza vituo vya Kikuletwa, Tosamaganga na Mbalizi, ili viweze kuchangia ipasavyo maendeleo ya sekta ndogo ya umeme.
This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.
Tuesday, November 13, 2007
TANESCO yaandaa mikataba kuuziana umeme
Posted by
Godfrey
at
09:58
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment