TANZANIA ipo katika mchakato wa kuanzisha mikataba kwa ajili ya miradi midogo midogo ya kuzalisha umeme usiozidi megawati 10.
Mkurugenzi wa Umeme wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Anastas Mbawala, alibainisha hilo jana alipozungumza na waandishi wa habari kuhusu uanzishaji wa miradi midogo midogo ya kuzalisha umeme inayotokana na maji, jua, mabaki ya bidhaa na upepo.
Alisema Tanzania ina vyanzo vingi vya kuzalisha, umeme lakini havijatumika ipasavyo na EWURA wamedhamiria kufufua utumiaji wa vyanzo hivyo kwa kuanza kuandaa mikataba iatakayokuwa bora zaidi na yenye kudhibiti vitendo vya rushwa na ufisadi wakati wa kuingia mikataba ya umeme.
Alisema mikataba ya miradi hiyo midogo midogo itaandaliwa na bei na mwekezaji atakuja nchini huku akijua thamani ya mradi na wala si kujadili gharama kama ilivyo hivi sasa.
“Tunayo maeneo mengi ambayo yanaweza kuzalisha umeme wa kutosha, lakini kutokana na kutokuwa kwa mipango mizuri ya uendelezaji na mikataba wananchi hukosa umeme kutoka katika vyanzo hivyo,” alisema Mbawala.
Alisema uandaaji wa makataba huo na uingiaji wa mkataba baina ya mwekezaji na serikali utajulikana kwa wananchi kwani watapata nafasi ya kutoa maoni yao ndani ya siku 21 na baada ya hapo EWURA itayachukua maoni hayo.
Aliongeza kuwa gharama hizo za mradi zitakuwa zikiangaliwa kila mwaka, ili kuendana na kupanda kwa gharama au mabadiliko ya aina yoyote ambayo hutokea mara kwa mara.
Alisema kampuni zinazozalisha umeme huo zitaweza kuuuza katika Shirika la Ugavi wa Umeme Tanzania (Tanesco) na kuingizwa katika gridi ya taifa na hivyo kusaidia kupunguza tatizo la kutokuwapo kwa umeme wa kutosha.
Alibainisha kuwa kukamilika kwa mchakato huo kutasaidia kwa kiasi kikubwa maeneo ya vijijini kupata umeme wa uhakika kwani kuna baadhi ya sehemu hawawezi kuzalisha umeme mwingi na kuliepusha taifa na matatizo ya uhaba wa umeme unaotokea mara kwa mara.
Source: Tanzania Daima, November 6, 2008
This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.
Sunday, November 09, 2008
Tanzania kuanzisha miradi ya uzalishaji umeme
Posted by
Godfrey
at
09:38
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment