This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.

Thursday, November 13, 2008

Pinda ataka wawekazajii wa umeme

WAZIRI Mkuu wa Tanzania, Mizengo Pinda amezita nchi wananchama wa Mamlaka za Udhibiti wa Huduma za Umeme Kusini mwa Afrika (Rera) kuvuta wawekezaji katika sekta ya umeme ili kuondoa tatizo kubwa la umeme linalozikumba nchi wanachama wa Jumuiya ya Biashara Kusini mwa Afrika (SADC).

Pinda aliishauri Rara kuweka mikakati imara

itakayozewezesha nchi wanachama kupunguza tatizo la upatikanaji wa nishati hiyo kwa sababu inawezekama juhudi na maarifa vikifanyika.

Waziri Pindi alitoa changamoto hiyo jana wakati akifungua Mkutano wa Tano wa Mwaka wa Rare unaofanyika katika

Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Arusha (AICC).

“Afrika ndiyo yenye kiwango kidogo cha upatikanaji wa umeme ambacho ni sawa na asilimia 25 tu, hali mbaya zaidi ni vijijini ambapo wakazi zaidi ya asilimia 75

huishi ambao hupata umeme wa asilimia mbili tu,” alisema Waziri.

Alitoa mfano wa Nchi za SADC ambazo zilipigania Uhuru wa Nchi hizo na kufanikiwa na kwamba iwapo Nchi hizo

zitaunganisha nguvu zao kwa kugawana vyanzo hivyo ni wazi watashinda.

Baadhi ya changamoto alizozitoa Waziri Mkuu katika kukabiliana na tatizo hilo ni kupanua huduma hizo kwa

kutumia nguvu za maji, makaa ya mawe, gesi asilia na mafuta.

Pia alizitaka nchi wananchama wa jumuiy hiyo kukabiliana na changamoto kadhaa kama uhaba fedha kwa ajili ya kugharamia miradi hiyo, ufundi, miundombinu na kuepukana na utegemezi zaidi katika umeme unaotokana na maji ambao sasa si wa uhakika.

Naye Waziri wa Nishati na Madini,

William Ngeleja alisema lengo kuu ni kuangalia ni jinsi ya kuunganisha nguvu katika kukabiliana na tatizo hilo.

“Ni wakati muafaka kwa nchi zetu kuhakikisha kwamba huduma

hiyo inaboreshwa na inakuwa endelevu,” alisema Ngeleja.

Awali, Mwenyekiti wa Bodi ya Mamla ya Udhibiti wa Maji na Nishati (Ewura), Simon Sayore alisema lengo ni kuhakikisha kuwa tatizo la uhaba wa umeme

katika nchi hizo.

Mkutano huo unawakutanisha wadau 150 wa kutoka nchi wanachana wa Rera na wasiowanachama kutoka nchi za Mozambique, Zambia, Malawi, Nigeria, Lesotho, Afrika Kusini, Namibia, USA, Norway, Madagascar, Angola,

Botwsana, Uganda, Kenya and Tanzania.

source: Mwananchi, November 13, 2008

No comments: