WAZIRI wa Nishati na Madini, Nazir Karamagi amesema atafurahi iwapo atasikia Kampuni binafsi ya kuzalisha umeme ya IPTL ikivunja mkataba wake na serikali.
Akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi ndogo za Bunge wakati wa kikao cha Kamati ya Bunge ya Uwekezaji na Biashara, Dar es Salaam jana, Waziri Karamagi alisema hatua hiyo itasaidia kupunguza mzigo wa kuilipa mamilioni ya fedha kampuni hiyo.
“Nitafurahi sana kama IPTL siku moja nikisia inavunja mkataba na serikali, kwa sababu tumekuwa tukitoa kiasi kikubwa cha fedha kwa ajili ya kuilipa kutokana na kuzalisha umeme kwa muda mrefu sasa,” alisema Waziri Karamagi.
Alisema jambo hilo ni la hiari na wala serikali haina mamlaka kwa vile IPTL bado ina mkataba wa miaka 11 na serikali katika uzalishaji wa nishati hiyo muhimu kwa matumizi ya wananchi.
“Hili ni suala la hiari kwa kuwa IPTL bado wana mkataba wa miaka 11 mbele yetu, lakini kwa sasa itaendelea na mkataba wake hadi ukapomalizika kama makubaliano yaliyopo yanavyoonyesha kwenye mkataba,” alisema Waziri Karamagi.
Kuhusu muswada wa sheria ya umeme, Waziri Karamagi alisema endapo utapitishwa na kuwa sheria, utasaidia serikali kupunguza mzigo mzito iliyonao katika uendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Alisema licha ya gharama za uwekezaji kwenye sekta ya umeme kuwa kubwa, ambapo kwa mwekezaji yeyote atataka kupata faida, jambo ambalo kwa hivi sasa haliepukiki.
Alisema ujio wa sheria mpya utasaidia kuondoa sheria iliyotungwa miaka mingi iliyopita, lengo likiwa ni kukabiliana na hali ya mageuzi ya kiuchumi.
Alisema mbali ya sheria hiyo, serikali imeanzisha chombo cha wakala wa usambazaji umeme vijijini ambacho kitakuwa na kazi ya kusambaza nishati ambacho kitakuwa kinapewa ruzuku na serikali.
Source: Tanzania Daima, jan 18, 2008
This blog contains information about what is happening in energy access development in Tanzania. You are welcome to give your thoughts and ideas on the issues published. Thank you.
Friday, January 18, 2008
Karamagi: Nitafurahi IPTL ikivunja mkataba
Posted by
Godfrey
at
07:56
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment